EXIM BIMA FESTIVAL PRESS CONFERENCE

EXIM BIMA FESTIVAL 2024: Burudani yenye Lengo la Kuboresha Huduma za Afya ya Akili
Dar es Salaam – Mwezi Septemba, Benki ya Exim Tanzania inawakaribisha Watanzania wote na wadau mbalimbali kujumuika pamoja kwa ajili ya jambo muhimu na la kipekee; Afya ya Akili. Ikiwa inasherehekea miaka 27 ya kuwahudumia Watanzania tangu kuanzishwa kwake, benki ya Exim inakuja na Exim Bima Festival 2024, ikiwa na kaulimbiu ‘Amsha Matumaini’, ambayo itafanyika mnamo tarehe 28 Septemba 2024 katika Viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam.
Hili ni zaidi ya tamasha, ni wito kwa kila Mtanzania kuchukua hatua kuongeza uelewa na msaada kwa watu wenye tatizo la afya ya akili.


